Baraka FM

TADIO yawanoa wahariri, wataalam wa kidijitali mikoa ya Nyanda za Juu Kusini

11 September 2023, 23:27

Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakifuatili kwa makini mafunzo wanayopewa. picha na Hobokela Lwinga

Katika kuimarisha na kupunguza changamoto zinazoikabili sekta ya habari nchini,TADIO imeendelea kuvijengea uzoefu vyombo vya habari ili kuondokana na mifumo ya analojia na kwenda kidijitali kulingana na mabadiliko ya ulimwengu.

Na Hobokela Lwinga

Wamiliki wa vyombo vya habari nchini wametakiwa kutumia vyema mitandao ya kijamii ikiwemo kuhabarisha umma ili kuimarisha maendeleo ya kiuchumi ya taasisi zao.

Wito huo umetolewa na afisa mradi wa shirika la habari la maendeleo  Tanzania Saum Bakari katika mafunzo yaliyowakutanisha wahariri na wakuu wa kidijitali kutoka mikoa mbalimbali ya Nyanda za Juu kusini yaliyoandaliwa na shirika hilo na kufanyika ktika ukumbi wa usungilo uliopo jijini Mbeya.

Bi. Saum amesema ili vyombo vya habari viweze kupata tija havina budi kutumia teknolojia kwani inasaidia kujitangaza.

Pichani ni afisa mradi kutoka TADIO Saumu Bakari akizungumza na wanahabari kuhusu umuhimu wa mafunzo na faida ya matumizi ya jukwaa la radiotadio.
Sauti ya afisa mradi wa TADIO bi Saum Bakari

Kwa upande wake mkufuzi kwenye mafuzo hayo Amua Rushita amesema mafunzo hayo yana lengo la kuwajengea uwezo wasimamizi wa vyombo vya habari ili kuweza kujiongezea wafuasi ndani na nje ya mikoa yao.

Katika picha ni mkufunzi wa mafunzo Bw. Amua Rushita akiendelea kutoa elimu kwa washiriki wa mafunzo.
Sauti ya Amua Rushita katika mafunzo yanayoendelea katika ukumbi wa Usungilo hotel Mbeya.

Nao baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo Lennox Mwamakula na Lusy Dashud wameahidi kwenda kuyafanyia kazi waliyofundishwa ikiwa ni pamoja na kuwezesha vyombo vyao kuanza kutumia fursa zilizopo kwenye mtandao wa TADIO.

Sauti ya baadhi ya washriki wa mafunzo wakieleza namna ambavyo wamenufaika na mafunzo yanayotolewa na TADIO Mbeya.