Baraka FM

Nchi 17 kufanya utafiti zao la mpunga nchini

23 January 2024, 08:43

Na mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde. Juma Zuberi Homera amefungua Mkutano wa Afrika ambao umeandaliwa na Tasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa zao la Mpunga Internation Rice Research Institute (IRRI) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Uyole wenye lengo la kuzindua utafiti juu ya mbegu mpya ya mpunga, mbegu itakayosaidia kuongeza tija kwenye zao hilo la mpunga.

Homera amesema baada ya skimu za umwagiliaji takribani 12 zilizojengwa mkoani Mbeya kukamilika ana uhakika kuwa uzalishaji wa mpunga utaongezeka kutoka tani laki sita mpaka milioni mbili na laki tano na hivyo kufanya soko la mpunga na mchele kutanuka zaidi hasa Tanzania, Afrika na dunia nzima.

Bi. Josephine Manase ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela yeye anaeleza namna ambavyo wakulima na wafanyabiashara wilayani humo watanufaika na mradi huo kwa kuwa wao ni miongoni mwa wazalishaji wa zao hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mh. Jaffary Hanniu anasema wamejipanga kufanya mageuzi ya kilimo hicho cha mpunga kupitia halmashauri ya Busokelo na tayari wamezungumza na timu ya umwagiliaji kuona namna ambavyo wanaweza kuchepusha mto Mbaka ili uwanufaishe pia wananchi wa wilaya ya Rungwe.