Baraka FM

Mercy World Organization yawa faraja kwa wanyonge

22 February 2024, 16:57

Na Hobokela Lwinga

Wadau, mashirika na watu binafsi wameombwa kujitokeza kusaidia makundi maalum ikiwemo yatima ili kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa bodi ya  taasisi isiyo ya kiserikali ya Mercy World Organization MEWO Subira Mwasamboma na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Mch.Dkt Tuntufye mwenisongole wakati wa hafla ya kukabidhi mahitaji ya shule na vyakula kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa mtaa wa Maanga kata ya ilomba vilivyotolewa na katika Ofisi za taasisi hiyo zinazopatikana katika viwanja vya John Mwakangale nanenane jijini Mbeya.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa WEWO Nicodemas Kennedy amesema taasisi yake kwa sasa inatekeleza mradi wake wa okoa maisha katika kata ya ilomba jijini mbeya huku akisema miaka ya karibuni wataongeza wigo wa kuhudumia na kata zingine.

Nico Alfred ni meneja mradi kwenye taasisi ya WEWO amesema katika utekelezaji wa mradi wamebaini uwepo wa wazazi kuuza misaada ambayo wamekuwa wakitoa sambamba na walimu kutokuwa waaminifu pindi taasisi hiyo inapopeleka misaada kwa watoto wanaosaoma kwenye shule zao.

Nao baadhi wanufaika wakiwemo wazazi na watoto wamelishukru shirika hilo kwa misaada ambayo wamekuwa wakiitoa kwao.

Katika ugawaji wa misaada hiyo wanufaika wameweza kupatiwa daftari,sare za shule pamoja na vyakula.