Baraka FM

Wanavyuo washauriwa kujiajiri na kuondokana na makundi maovu

7 November 2023, 12:25

Baadhi ya wanafunzi wahitimu wa chuo cha ufundi Moravian(picha na Deus Mellah)

Vijana wa rika mbalimbali  wanaomaliza masomo yao kwenye vyuo tofauti nchini wametakiwa kutojiingiza katika makundi yasiyofaa kwani yanaweza kukatisha ndoto zao za baadaye.

Na Deus Mellah

Wito huo  umetolewa na msimamizi wa miradi kanisa la Moravian jimbo la Kusini Magharibi Esau Swila wakati akizungumza katika mahafali ya wanafunzi wa kikristo yaani University  Student  Christian Fellowship USCF katika Chuo cha Ufundi Moravian jijini Mbeya.

Amesema vijana wengi wakimaliza vyuo mbalimbali  wakirudi nyumbani kwao wakati  wanasubiri ajira huwa wanajiingiza katika makundi yasiyofaa kama vile uvutaji wa bangi kucheza kamali na kujihusisha kwenye mahusiano hali inayosababisha kutotimiza malengo yao.

Msimamizi wa miradi kanisa la Moravian jimbo la Kusini Magharibi Esau Swila(picha na Deus mellah)
Sauti ya Msimamizi wa miradi kanisa la Moravian jimbo la kusini magharibi Esau Swila

Kwa upande wake mratibu  wa vyuo vikuu na kati vilivyopo mkoa wa mbeya na songwe mch  Whisper  Siwiti   amewataka vijana   hao kufanya kazi za kujiajiri    ili waweze kujiingizia kipato kwani wamepata  uzoefu wa fani mbalimbali.

Mratibu  wa vyuo vikuu na kati vilivyopo mkoa wa mbeya na songwe mch  Whisper  Siwiti(picha na Deus Mellah)
Sauti ya Mratibu  wa vyuo vikuu na kati vilivyopo mkoa wa mbeya na songwe mch  Whisper  Siwiti

Naye rais wa chuo cha ufundi   Moravian ambaye pia ni kiongozi wa USCF Crein Mlomba amesema kile walichofundishwa  na walimu wao kuhusu masuala ya ufundi  wataendelea kuyafanyia kazi maana ndo hazina yao ya baadae.

Sauti ya Rais wa chuo cha ufundi   Moravian ambaye pia ni kiongozi wa USCF Crein Mlomba

Nao baadhi ya wanafunzi wa chuo cha ufundi Moravian wamesema kuwa wakieenda mtaani watahakikisha wanafanya shughuri mbalimbali  zinazoweza kuwaingizia kipato na kuachana na kujiingiza katika makundi yasiyofaa.

Sauti ya baadhi ya wanafunzi wa chuo cha ufundi Moravian