Baraka FM

Mch. Mbazzah astaafu, aagwa na Baraka fm radio

1 February 2024, 17:12

Mch.Nehemia Mbaza(mbele suti ya bluu)akichukua chakula katika hafla ya kumuaga(picha na Hobokela Lwinga)

Na Hobokela Lwinga

Kituo cha redio Baraka kimemuaga mfanyakazi wake mchungaji Nehemia Mbaza baada ya kustaafu kukitumikia kituo hicho kwa muda wa miaka 13.

Hafla ya kumuuaga mchungaji huyo imefanyika katika ukumbi mdogo wa chuo cha ufundi moravian uliopo kadege jijini mbeya.

wafanyakazi wa Baraka fm katika picha ya pamoja(picha na Hobokela Lwinga)

Akizungumza katika hafla hiyo meneja wa radio Baraka Charles Amlike amesema ni vyema kila mtu ajitathimini katika utendaji wake wa kazi kabla ya kustaafu kwake kwani kila mtu ni lazma astafu kulingana na miongozo katika taasisi anayofanya kazi.

Aidha amlike amemtaka mchungaji huyo kuendelea kukiombea kituo mahala popote anapokuwa.

Meneja wa radio Baraka Charles Amlike (Picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya meneja wa radio Baraka Charles Amlike

kwa upande wake mchungaji Gama Simbowe ambaye ni maratibu wa vipindi vya neno la mungu ambaye pia amekuwa akifanya kipindi pamoja cha ijue biblia amesema mchungaji mbaza kwake ni mwalimu katika mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya kujibu maswali redioni.

watangazaji wa baraka fm radio wakila chakula cha pamoja (picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mchungaji Gama Simbowe

Nae Mkuu Wa Vipindi Radio Baraka Radio Mpoki Japhet Amesema Mch Mbaza  Alikuwa Na Mchango Mkubwa Katika Radio Kwani Ni Miongoni Mwa waanzilishi wa radio.

Mkuu Wa Vipindi Radio Baraka Radio Mpoki Japhet(picha na Hobokela Lwinga)

Sauti ya Mkuu Wa Vipindi Radio Baraka Radio Mpoki Japhet

Baadhi Ya Wafanyakazi Waliofanya Kazi Na Mchungaji Mbaza Wamesema mchungaji mbaza alikuwa msaada mkubwa kwa kituo kutokana na utendaji kazi wake huku wakijivunia upendo alikuwa nao kwa kila mfanyakazi.

Mtangazaji Rukia (Chasanika aliyesimama) na Josea Sinkala (aliyekaa)-picha na Hobokela Lwinga
Sauti za Baadhi Ya Wafanyakazi Waliofanya Kazi Na Mchungaji Mbaza

Hata hivyo mchungaji Nehemia Mbaza ameishukru taasisi ya radio Baraka kwa kuwa nae begakwabega kipindi chote alichofanya kazi kama mtangazaji.

Mchungaji Nehemia Mbaza(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mchungaji Nehemia Mbaza