Baraka FM

Rungwe DC yakamilisha ujenzi nyumba za watumishi

18 January 2024, 20:59

Na Hobokela Lwinga

Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imekalisha ujenzi wa nyumba ya watumishi (two in one) katika shule ya sekondari Msasani one kwa gharama ya shilingi million 100.

Fedha hii imetolewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Kukamilika kwa nyumba hii kumesaidia kuondoa changamoto ya makazi kwa Watumishi na hivyo kuwa karibu na shule hatua itakayosaidia kutoa elimu bora na stahiki kwa wanafunzi .

Shule ya sekondari Msasani one Imejengwa kwa gharama ya shilingi million 470 fedha zilizotolewa na serikali kupitia mpango wa SEQUIP.

Fedha hizi zimejumuisha ujenzi wa vyumba vya madarasa, maktaba, Maabara,TEHAMA , Vyoo na jengo la Utawala