Baraka FM

Bodaboda Mbeya wagoma, wavamia ofisi za jiji

22 February 2024, 17:35

Na Ezra Mwilwa

Umoja wa madereva bodaboda mkoa wa Mbeya wamefanya maandamano katika ofisi za jiji kuomba kusikilizwa kero zao ikiwepo kukamatwa na kutozwa faini wawapo barabarani.

Mwenyekiti wa umoja huo Ndg. Aliko Fuanda amesema wamekuwa wakikamatwa pindi wanapoingia soko jipya la Mwanjelwa na kutozwa faini kutoka LATRA.

Mwenyekiti wa Umoja wa bodaboda jiji la Mbeya Ndg.Aliko Fuanda
Sauti ya Mwenyekiti wa Umoja wa bodaboda jiji la Mbeya Ndg.Aliko Fuanda

Nao baadhi ya viongozi Mbalimbali wa vituo vya Bodaboda wamesema walipeleka malalamiko kwa kiongozi wa jiji nayeye alienda Kwenye uongozi wajiji hakupewa ushirikiano hali iliyo sababisha kufanyika kwa maandamano hayo.

Sauti za baadhi ya viongozi Mbalimbali wa vituo vya Bodaboda

Baada ya kufanya maandamano hayo hadi ofisi za jiji hakuna kiongozi wa Serikali alie jitokeza kusikiliza Kelo zao hali iliyo peleakea mwenyekiti Oswad Fuanda kutoa Tamko kwa Bodaboda wote kuto kukamatwa na kutozwa faini mpaka watakapo patiwa Ufumbuzi wa kelo zao.

Sauti ya Mwenyekiti wa Umoja wa bodaboda akitoa tamko Ndg.Aliko Fuanda

kituo hiki kimemtafuta mkurugenzi wa jiji la Mbeya John Nchimbi ili kujua sababu za malalamiko ya madeva hao lakini jitihada hizo zimegonga mwamba kutokana na kiongozi huyo kuwa kwenye kikao.