Baraka FM

Walimu 20 Mbeya kunufaika na mafunzo, kupatiwa ajira

21 September 2023, 16:17

Baadhi ya vijana wakimsikiliza MNEC wa CCM katika ukumbi wa Beaco Mbeya(picha na Rukia Chasanika)

Kutokana na vijana wengi kuwa na taaluma za fani mbalimbali bado suala la ajira limekuwa changamoto kwa makundi mbalimbali ya vijana hivyo wadau wanapaswa kuangalia hilo hasa walio kwenye sekta binafsi kutoa fursa ya ya ajira kwa vijana hao

Na Rukia Chasanika

Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa kupitia mkoa wa Mbeya na mkurungezi wa shule za paradise mission na patrick missioni Ndele Mwaselela ametoa fursa ya kuajiri walimu ishirini wa lugha kupata mafunzo na kwenda kufundisha mafunzo ya awali(pre form one) kwa wanafunzi waliomaliza darasa la saba katika wilaya ya Mbeya,Halmashauri ya Mbeya vijijini na wilaya Chunya bila malipo.

Mwaselela amesema hayo wakati akishiriki chakula cha pamoja na vijana wa mkoa wa Mbeya wa kada mbalimbali ambapo amejitolea kuwalipa walimu mshahara ndani ya miezi mitatu ya kuwafundisha wanafunzi wanaojiandaa kuanza kidato Cha kwanza mwakani ambao watasoma Bure(pre_form one).

Aidha Mwaselela amesema vijana wanatakiwa kudhubuti kwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa serikali za mitaa ambao utawasaidia kuwafikisha katika hatua   za uongozi wa juu zaaidi.

Ameongeza kuwa katika ulimwengu huu wa taknolojia vijana wanatakiwa kutumia teknolojia kwa simu zao ili kujiingiza kipato badala ya kutuma picha zisizo na maana katika mitandao ya kijamii.

MNEC wa CCM ndele Mwaselela(picha na Rukia Chasanika)
sauti ya MNEC wa CCM ndele Mwaselela

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki Ezekiel Kamanga amesema vijana wanatakiwa kutokata tamaa katika utafutaji wa maisha kwani watu wote waliofanikiwa kuna changamoto walipitia lakini waliendeleza ndoto zao.

Vijana wakifuatilia maongezi ya MNEC wa CCM Ndele Mwaselela(picha na Rukia Chasanika)
Sauti ya Ezekiel Kamanga