Baraka FM

TADIO yawaasa wanahabari kutumia kalamu zao kwa weledi

25 April 2024, 20:41

Mkufunzi kutoka mtandao wa Redio Jamii Tanzania TADIO Hilali Ruhundwa (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha redio Baraka cha jijini Mbeya

Kufuatia ukuaji wa sayansi na teknolojia duniani, tasnia ya habari ni moja ya tasnia inayotakiwa kwenda sambamba na mabadiliko hayo katika kuzingatia taaluma yao kuwa karibu na jamii wanayoitumikia kwa kuwalisha habari zenye ukweli na uhakika.

Na Hobokela Lwinga

Waandishi wa habari nchini  wametakiwa kutumia kalamu zao kwa weledi na kufuata maadili ya taaluma yao kutokana na taaluma hiyo kuaminiwa kwa kiasi kikubwa na jamii.

Wito huo umetolewa na mkufunzi Hilali  Ruhundwa  kutoka mtandao wa redio jamii wa TADIO wakati akitoa mafunzo kwa watangazaji na waandishi wa habari wa  kituo cha redio Baraka FM kilichopo Kadege jijini Mbeya. 

Ruhundwa amesema misingi ya taaluma ya uandishi wa habari ni kuandika kitu chenye ukweli na uwazi.

Mkufunzi Hilali  Ruhundwa  kutoka mtandao wa redio jamii wa TADIO akitoa mafunzo kwa wanahabari wa Baraka FM (Picha na Hobokela Lwinga)

 

Sauti ya Hilali Ruhundwa akiwakumbusha wanahabari miiko yao.

Aidha Ruhundwa amesisitiza kuwa kuelekea kipindi cha uchaguzi waandishi wa habari wazingatie usawa wa kutoa habari kwa vyama vyote vya siasa vitakavyoshiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa  2024 na uchaguzi mkuu 2025.

Sauti ya Hilali Ruhundwa akiwaasa waandishi wa habari.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wafanyakazi, meneja wa redio Baraka FM Charles Amulike amewataka washiriki kuzingatia mafunzo waliyoyapata.

Meneja wa redio Baraka FM Charles Amulike (Picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya meneja wa Redio Baraka FM Charles Amulike

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo kwao yameongeza chachu ya utendaji katika kutekeleza majukumu yao ya kuuhabarisha umma.

Sauti za baadhi ya waandishi wa redio baraka walio patiwa elimu maalumu