Baraka FM

Vyombo vya habari vyatakiwa kuibua changamoto katika jamii

12 September 2023, 11:11

Meneja wa radio Baraka Charles Amulike akiwa anatoa msaada wa vifaa vya shule katika shule ya msingi Ilota Mbeya vijijini (picha Hobokela Lwinga)

Vyombo vya habari vimekuwa vikiaminiwa kuwa na mchango wa kuibua changamoto mbalimbali katika jamii kutokana na hilo vinaoaswa kutumia wajibu wake kuwa chanzo cha kutatua kero zinazowakabili wananchi.

Na Rukia Chasanika

Vyombo vya habari mkoani Mbeya vimeoshauriwa kuibua changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii ili Serikali iweze kuzipatia ufumbuzi.

Hayo yameelezwa na Meneja wa kituo cha Radio Baraka cha jijini Mbeya Charles Amulike wakati wa zoezi la utoaji wa vifaa muhimu kwa wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Ilota iliyopo Mbeya vijijini.

Sauti meneja radio Baraka Charles Amulike

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ilota Joel Munuo amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mwalimu wa kike kwa miaka kumi, upungufu wa madarasa, vyoo na nyumba za walimu.

amesema tunakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mwalimu wa kike kwa miaka kumi, upungufu wa madarasa, vyoo na nyumba za walimu.

Sauti mwalimu mkuu shule ya msingi Ilota Joel Munuo

Hata hivyo Afisa elimu Kata ya Mshewe Yuda Kilawa amesema mchakato wa kumpata mwalimu wa kike ulikuwa unakwamisha na ukosefu wa nyumba za walimu amesema kwasasa utakamilika kutokana na uwepo wa nyumba mbili walimu zilizojengwa.

Sauti afisa elimu kata ya Mshewe Yuda Kilawa

Nae Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilota Musa Jek ameupongeza uongozi wa Radio Baraka na wadau mbalimbali kwa kufanikisha tukio hilo.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji cha Ilota Musa Jek

Ipi Kauli Ya Wanafunzi Walipewa Msaada Huo….

Baadhi ya wananfunzi wa shule ya msingi Ilota wakifurahia zawadi za daftali walipewa na radio baraka

Sauti za wanafunzi shule ya msingi Ilota