Baraka FM

Zimamoto Mbeya yawafikia wafanyabiashara sokoni na kutoa elimu ya kuzima moto

14 September 2023, 13:39

Pichani ni wafanyabiashara wa soko la Igawilo jijini Mbeya wakiendelea na taratibu za kufanya biashara sokoni hapo (picha na Ezra Mwilwa)

Elimu ni msingi wa kuongeza maarifa na ili uwe na amaarifa huna budi kuifunzz kwa waliofanikiwa kutkana na umhimu wa elimu jeshi la zimamoto haliko mbali na wananchi katika kuwapatia elimu pasipo kubagua rika,rangi,kabila wala umbo la mtu.

Na Ezra Mwilwa

Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Mbeya limebaini uwepo wa baadhi ya makundi ikiwemo masokoni kutokuwa na elimu ya vifaa vya kuzimia moto hali iliyopelekea kuyafikia makundi hayo na kutoa elimu.

Akitoa elimu katika soko la igawilo lilipo jiji Mbeya afisa habari wa jieshi nla zimamoto na uokoaji Coplo Ester Kinyaga amesema wanaowajibu wakuhakikisha kila mwananchi anafahamu matumizi sahihi ya vifaa vya kuzimia moto.

Katika hatua nyingine Coplo Ester amewataka wananchi kutoa taarifa ya pindi wanapoona matukio ya moto na mengine yanahitaji uokozi ikiwemo kudumbukia.

Afisa habari zimamoto na uokoaji Mbeya Coplo Ester Kinyaga akiendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara katika soko la Igawilo jijini mbeya(Picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya afisa habari zimamoto na uokoaji Ester Kinyaga

Nao baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Igawilo kutoka soko hilo wamelipongeza jeshi la Zimamoto kwakutoa elimu hiyo Pia wamesema walikua wakiona vifaa hivyo vimefugwa pasipo kujua matumizi yake.

Wafanyabiashara wa soko la Igawilo jijini mbeya wakifuatilia elimu ya uzimaji moto inayotolewa na afisa habari wa jeshi hilo Coplo Ester Kinyaga baada ya kuwatembelea sokoni hapo
Sauti za wananchi kutoka soko la igawilo jijini mbeya

Jeshi la zimemoto na uokoaji mkoa wa mbeya limekuwa na utaratibu wa kuwatembelea wananchi kwenye maeneo yao na kuwakusanya na kisha kutoa elimu kwenye mikutano ya hadhara.