Baraka FM

Coplo Kinyaga:Mnaweza kuisaidia jamii kuwa salama na majanga

17 November 2023, 21:21

Baadhi ya wanahabari walioshiriki mafunzo ya zimamoto na uokoaji mbeya kutoka baraka fm radio kulia ni Sifael kyonjola na Ezekiel Kamanga(kushoto)

Na Sifael kyonjola

Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mbeya limetoa mafunzo kwa waandishi wa habari jinsi ya kukabiliana na majanga ya moto yanapotokea katika jamii inayowazunguka.

Mafunzo hayo yametolewa na afisa habari   zimamoto na uokoaji mkoa wa Mbeya Koplo Ester Kinyaga katika ofisi za chama cha waandishi wa habari mkoani Mbeya.

Kinyaga amesema mafunzo hayo yametolewa kwa lengo la kuwapatia mafunzo waandishi wa habari juu ya elimu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga majanga mbali mbali yanapotokea katika shughuli zao.

Afisa habari   zimamoto na uokoaji mkoa wa Mbeya Koplo Ester Kinyaga (picha Sifael Kyonjola)
Sauti ya afisa habari   zimamoto na uokoaji mkoa wa Mbeya Koplo Ester Kinyaga

Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Mbeya Nebati Msokwa  amesema  kupitia mafunzo hayo waaandishi wa habari wamejifunza kuwa uokozi ni pamoja na kusaidia wajawazito waliokosa msaada,watu waliokumbwa na mafuriko pamoja na ajali ya moto.

Sauti ya Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Mbeya Nebati Msokwa 

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Emanuel Lengwa na mwanaisha makumbuli wamesema mafunzo yaliyotolewa ni pamoja na uokoaji wa wanyama wanapopata shida ya kutumbukia kwenye mito  na mashimo ambapo mwananchi anatakiwa  kutumia bure namba ya simu 114 kutoa taarifa mapema kwa  kikosi cha jeshi la zimamoto na uokoaji ili apate msaada.

wanahabari kushoto ni Mwanaisha Makumbuli na kulia ni Albart Msole
Sauti za washiriki wa mafunzo hayo Emanuel Lengwa na Mwanaisha makumbuli