Baraka FM
Baraka FM
21 July 2026, 05:32

Upendo kwa wasiojiweza hujengwa kwa matendo kwa watoto yatima na watu wenye mahitaji.
Na Ezra Mwilwa
Umoja wa Watoto wa Wachungaji wa Kanisa la Moravian mkoa wa Mbeya umewatembelea watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha Amani Nsalaga, kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian jimbo la kusini Magharibi.
Wanaumoja hao, wakiongozwa na mwenyekiti wao, Ndugu Benjamin Mwambafu, wamesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuwasaidia watu wenye uhitaji katika jamii na kuendelea kuonesha upendo kwa makundi mbalimbali yenye mahitaji.
Mchungaji mlezi wa kituo hicho, Bahati Mshani, amewashukuru wanaumoja hao kwa kufika katika kituo hicho na kutoa sadaka pamoja na misaada mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaolelewa hapo.

Nao baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wamewashukuru wanauoja huo kwa msaada walioutoa, huku wakitoa wito kwa watu mbalimbali kujitokeza na kufika katika kituo hicho ili kuwasaidia watoto yatima na wenye mahitaji.