Baraka FM

Waziri mkuu,tumieni kiswahili kwenye shughuli zenu

18 March 2024, 19:51

Viongozi na waandaaji wa kongamano wakiwa kwenye picha ya pamoja na waziri mkuu Kassim Majaliwa(Picha na Hobokela Lwinga).

Waziri Mkuu kassim Majaliwa amewataka watanzania kutumia fursa ya matumizi sahihi ya lugha ya kiswahili ili kujipatia ajira kutokana na mataifa mengine kuipokea lugha hiyo kwa kasi kubwa.

Na Hobokela Lwinga

Waziri mkuu ameagiza watanzania na ofisi za Serikali kuhakikisha wanatekeleza matumizi ya lugha ya kiswahili yanatekelezwa ikiwa ni pamoja na kuandika nyaraka za Serikali,warsha, makongamano kutumia lugha ya kiswahili katika utekelezaji wa majukumu yao.

Waziri mkuu ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la nne la Idhaa za kiswahili Dunia linalofanyika katika ukumbi wa hotel ya Edeni jijini Mbeya.

Waziri Mkuu kassim Majaliwa(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Waziri Mkuu kassim Majaliwa

Nao mawaziri Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo wa Tanzania Dkt.Damas Ndumbaro na Tabia Maulid Mwita Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo wa Zanzibar wamesema wametumia mziki,sanaa na michezo kukuza kiswahili huku wakisema wataendelea kutoa ushirikiano wa kukuza kiswahili ndani na nje ya nchi.

Waziri Mkuu kassim Majaliwa akitembelea baadhi ya maonyesho katika kongamano la idhaa za kiswahili duniani (picha na Hobokela Lwinga)
Sauti za mawaziri Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo wa Tanzania Dkt.Damas Ndumbaro na Tabia Maulid Mwita Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo wa Zanzibar.

Katibu mkuu baraza la kiswahili la taifa BAKITA Consolata Mushi amesema kongamano hilo limehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wamiliki wa vyombo vya habari,watozi wa mziki,wanahabari,walimu na Wanafunzi wa uandishi wa habari huku akisema kongamano hilo litakuwa na mawasilisho mbalimbali kama vile matumizi sahihi ya lugha ya kiswahili kwa vyombo vya habari.

Sauti ya Katibu mkuu baraza la kiswahili la taifa BAKITA Consolata Mushi

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mbeya mhe.Juma Zuberi Homera akiwakaribisha washiriki mkoani kwake amesema uwepo wa kongamano hilo kutaisaidia kuongezeka kwa frusa za uwekezaji sambamba na kujionea vivutio vya utalii.

Kwenye picha kushoto ni Ivillah Mgala mwandishi wa habari Baraka Fm redio akifuatilia kwa makini mawasilisho katika kongamano la idhaa za kiswahili dunia (picha na Hobokela Lwinga).
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Mbeya mhe.Juma Zuberi Homera

Hata hivyo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge amesema viongozi wa nchi waliona mbali kwani lugha ya kiswahili imekuwa sababu kubwa ya usalama wa nchi.

Baadhi ya washiriki wa kongamano la idhaa za kiswahili duniani(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge

“Katika kongamano hilo la nne linalofanyika mkoani Mbeya linakwenda na kauli mbiu isemayo Tasinia ya habari na fursa za ubidhaishaji kiswahili dunia.”