Baraka FM

Wachimbaji wadogo wa madini Chunya walia na mercury, wapata ulemavu

30 October 2023, 16:01

Wachimbaji wadogo wa eneo la Itumbi kata ya Matundasi wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wakimsikiliza Waziri wa Madini Anthony Mavunde (picha na Hobokela Lwinga)

Teknolojia ni jambo zuri katika ulimwengu wa sasa lakini hali imekuwa tofauti kwa wachimbaji eneo la Chunya ambapo badala ya furaha imegeuka kilio.

Na Hobokela Lwinga

Wachimbaji wadogo wa madini katika  eneo la Itumbi kata ya Matundasi wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wameiomba serikali kuwatazama kwa jicho la tatu kwa kuwatatulia  changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kuwasogezea huduma za afya jirani pamoja na kuwapatia mikopo itakayowawezesha kuendesha shughuli zao za uchimbaji.

Wachimbaji hao wameeleza kilio chao mbele ya Waziri wa Madini Anthony Mavunde ambaye amefanya ziara ya kikazi katika eneo hilo iliyokuwa na lengo la kutembelea migodi na kuzungumza na wachimbaji wadogo, wauzaji, wanunuzi pamoja na kutatua kero zinazowakabili.

Sauti za wachimbaji madini chunya mbeya

Naye mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM mkoa wa Mbeya Yasin Ngonyani amesema tatizo linalowakabili wachimbaji wadogo katika eneo la Itumbi na maeneo mengine ni suala la mitaji, vitendea kazi kwani kwa sasa bado wanatumia teknolojia ya chini haileti tija kwao na taifa pia.

Sauti ya Mwenyekiti wa Umoja Wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Ccm Mkoa Wa Mbeya Yasin Ngonyani

Akijibia changamoto hizo Waziri mwenye dhamana ya madini Anthony Mavunde amesema kutokana na wachimbaji wengi kuchimba  madini kwa kubahatisha kutokana na kukosa taarifa wizara kwa kushirikiana na wataalam wameanza mchakato wa kuboresha taasisi ya jiolojia na utafiti wa madini  ili wananchi wasichimbe madini kwa kubahatisha.

Mhe. Anthony Mavunde Waziri wa Madini akizungumza na wananchi na wachimbaji Chunya mkoani Mbeya (Picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Waziri wa Madini Anthony Mavunde