Baraka FM

Mashamba ya shule yatumike kuimarisha lishe kwa wanafunzi

15 November 2023, 17:29

Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Momba, Bi. Regina Bieda(picha na mwandishi wetu)

Na mwandishi wetu

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Momba, Bi. Regina Bieda amewaagiza wakuu wa shule na waalimu wakuu kuhakikisha wanatumia vizuri ardhi ya shule kwa kulima mazao mbalimbali ya kuimarisha lishe bora kwa wanafunzi.

Bi. Regina Bieda ametoa agizo ilo wakati wa kikao kazi cha tathimini ya lishe kilichofanyika novemba 14 na kuweka mikakati ya kuimalisha afua za lishe kwa Halmashauri ya Momba. 

“Saizi ndio msimu wa kilimo umeanza na shule zetu nyingi zina ekari za kutosha za kuweza kulima mazao mbalimbali kwa ajili ya chakula na sisi tunahimiza sana mahindi lishe tunaamini yatakwenda kuboresha lishe kwa wanafunzi wetu” Bi. Regina Bieda.

Pia, Mkurugenzi wa Halmashauri, Bi. Regina Bieda ametoa wito kwa uongozi wa shule kwa kushirikiana na uongozi wa vijiji wahakikishe kila shule inatoa chakula bora kwa wanafunzi ili kuimarisha lishe zao.