Baraka FM

Mwenyekiti UVCCM Mbeya awataka vijana kutumia fursa zinazotolewana serikali

7 November 2023, 12:55

Vijana mkoani Mbeya wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuzitumia fursa mbalimbali ambazo zinatangazwa na serikali kwa lengo la kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Na Ezra Mwilwa

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Yassin Ngonyani baada ya kuwatembelea vijana wanaounda umoja huo wilayani kyela.

Ngonyani amesema ni wajibu wa kila kongozi kuwapigania vijana kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili sambamba na kusimamia mipando ya chama kikamilifu.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Yassin Ngonyani(picha na Ezra Mwilwa)

Kwa upande wake mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Kyela Basini Mwaipaja wameiomba serikali kutatua kero zao ikiwemo pikipiki zao kukamatwa na suala la utozwaji ushuru kwa mizigo isiyozidi tani moja.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Yassin Ngonyani akiwa na viongozi wengine wa UVCCM mkoa wa Mbeya