Baraka FM

Mjane mwenye watoto sita kupata nyumba kutoka taasisi ya Tulia Trust

21 March 2024, 09:07

Zoezi la kushusha tofari ujenzi wa nyumba ya mjane (picha na Ezra Mwilwa)

Mjane aliyekuwa akiishi kwenye nyumba ya maturubai Mbeya ameonwa na jicho la mbunge na spika wa Tanzania Dkt.Tulia Mwansasu Ackson ambaye pia ni Rais wa IPU baada ya kuishi kwa muda mrefu kwenye nyumba yenye maturubai.

Na Ezra Mwilwa

Taasisi ya Tulia Trust imeanza kumjengea nyumba ya kuishi Bi.Singwava Jackson mjane mkazi wa mtaa wa Itanji kata ya Iganjo jijini Mbeya aliyekuwa akiishi kwenye nyumba ya maturubai na watoto wake sita.

Mafundi wakiendelea na mikakati ya Ujenzi wa nyumba(picha na Ezra Mwilwa)

Ujenzi wa nyumba hiyo unatarajiwa kukamilika mwezi wa April mwaka huu na itakabidhiwa na Mkurugenzi wa Tulia Trust ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya mjini Mhe. Dr. Tulia Ackson.

Baadhi ya watumishi wa Tulia Trust wakiendelea kusogeza matofali ya ujenzi wa nyumba (picha na Ezra Mwilwa)

Kwa upande wake afisa habari wa taasisi hiyo Joshua Edward ametoa wito kwa jamii kusaidia watu wenye uhitaji.

Joshua Edward akitoa maelekezo(kulia) picha na Ezra Mwilwa