Baraka FM

Machinga Mbeya waitwa kujisajili

6 April 2024, 12:33

Mwenyekiti wa Umoja wa Machinga mkoa wa Mbeya (picha na Ezra Mwilwa)

Katika hali isiyo ya kawaida Mkoa wa Mbeya wafanya Biashara wadogo maarufu kama Machinga bado hawajapatiwa vitambulisho vya kufanya biashara zao.

Na Ezra Mwilwa

Wafanya Biashara wadogo maarufu kama Machinga mkoa wa Mbeya wametakiwa kujitokeza kufanya usajili wa kupata vitambulisho

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Machinga mkoa wa Mbeya Ndugu Jerry Mwatebela wakati akizungumza na kituo hiki Amesema wafanya Biashara wadogo maarufu kama Machinga wajitokeze kujiandikisha ili wapate vitambulisho maalumu watakavyo vitumia kwa Miaka mitatu.

Sauti ya Mwenyekiti wa Umoja wa Machinga mkoa wa mbeya Ndugu Jerry Mwatebela

Mwatebela Ameongeza kuwa wanaomba ushirikiano kutoka kwa Maafisa Maendeleo wote mkoani hapa kusaidiana na viongozi wa Machinga kukamilisha suala hilo kwa wakati mwafaka.

Mwenyekiti machinga Mkoa wa Mbeya Jerry Mwatebela aakieleza changamoto ya usajili wa wafanya Biashara (picha na Ezra Mwilwa)

Nae mwenyekiti wa Machinga Jiji la Mbeya Waziri Hemed amesema mpaka sasa wao wapo tayari kama viongozi kufanya usajili wa wanachama isipo kua changamoto ni ukosekanaji wa Elimu kwa Machinga na ushirikiano kutoka kwa maafisa Maendeleo wa Jiji.

Mwenyekiti Machinga Mbeya jiji Waziri Hemed(picha na Ezra Mwilwa)