Baraka FM

Mbunge Sikonge Tabora aipongeza halmashauri ya Rungwe Mbeya

12 December 2023, 19:23

Mheshimiwa Joseph Kakunda Mbunge wa  Jimbo la Sikonge Mkoa wa Tabora(Na mwandishi wetu,Rungwe Mbeya)

Na mwandishi wetu,Rungwe Mbeya

Mheshimiwa Joseph Kakunda Mbunge wa  Jimbo la Sikonge Mkoa wa Tabora ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa Kuzalisha zaidi ya  lita  za maziwa million 44 kwa mwaka hatua iliyoongeza kipato cha wananchi sambamba na uboreshaji wa Maisha yao.

Pongezi hizo amezitoa  leo tarehe 12.12.2023 wakati wa mawasilisho ya namna Wilaya ya Rungwe ilivyofanikiwa katika uboreshaji wa mifugo na ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Viongozi mbalimbali kutoka Wilaya ya Sikonge wamefanya ziara katika wilaya ya Rungwe lengo likiwa ni kujifunza namna bora ya Ukusanyaji wa mapato, Usimamizi wa miradi ya Maendeleo, sekta ya Kilimo na Mifugo, elimu, Viwanda pamoja na Utalii.