Baraka FM

Wachungaji kemeeni mambo ya ushoga unaoendelea duniani

8 April 2024, 20:02

Mchungaji Isac Mbwaga akiwasilisha mada ya kukemea ushoga (Picha na Ezra Mwilwa)

“Tumieni elimu na maarifa mliyoyapata vyuoni kuuaminisha ulimwengu juu ya imani ya kumtegemea Mungu na siyo fedha.”

Na Ezra Mwilwa

Wachungaji waliopo masomoni Chuo Kikuu Teofilo Kisanji na Chuo cha Itengule Mbeya wametakiwa kuendelea kukemea maswala ya ushoga yanayoendelea duniani.

Wito huo umetolewa na Kasisi wa kanisa la Angilikan Dayosisi ya Southern Canon Isac Mbwaga katika Chuo cha Utengule wakati akiwasilisha mada iliyokuwa imelenga kuwajenga wachungaji wanafunzi kufundisha kweli juu ya mambo ya ushoga.

Kasisi wa kanisa la Angilikan Dayosisi ya Southern Canon Isac Mbwaga (picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya Kasisi wa kanisa la Angilikan Dayosisi ya Southern Canon Isac Mbwaga

Nao baadhi ya wathiolojia walioshiriki katika mdahalo huo wamesema kama wachungaji wasiogope kusema kweli na kufundisha watoto walio shuleni na maeneo mbalimbali.

Wachungaji waliopo masomoni Chuo kikuu Teofilo Kisanja na Utengule
Sauti za wachungaji waliopo masomoni Chuo kikuu Teofilo Kisanja na Utengule

Kwa upande wao wachungaji Mhadhiri na Mchungaji wa Ushirika wa Teku Ekisa Shibanda na Makamu wa chuo cha Utengule mchungaji Tulinagwe Kibona wamesema ni vyema kila mtumishi anapopata nafasi ya kufundisha mahali popote aendelee kukemea suala la ushoga.

(Kushoto) wachungaji Ekisa Shibanda na Mchungaji Tulinagwe Kibona
Sauti za wachungaji Ekisa Shibanda na Mchungaji Tulinagwe Kibona