Baraka FM

Homera: Epukeni matumizi ya simu wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa

18 September 2023, 19:47

Baadhi ya wahudumu wa afya katika hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya wakifurahia mazungumzo ya mkuu wa mkoa Juma Zuberi Homera (Picha na Castus bhusolo)

Kufanya kazi kwa weledi ni sehemu ya binadamu anayejitambua na kutambua nafasi yake na ukitaka kupongezwa ni lazima uoneshe weledi wa kazi yako, ishi ukijua maisha yako yanategemea maisha ya mwingine.

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera leo Septemba 18 2023 amekutana na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na kufanya nao mazungumzo yaliyolenga kutambua mchango wao katika sekta ya afya ambapo moja ya vitu alivyosisitiza ni uadilifu na nidhamu katika utendaji kazi.

Aidha amewataka wafanyakazi wa hospitali hiyo kutunza vifaa vya hospitali vinavyotolewa na serikali  na kuepuka matumizi mabaya na uharibifu wa maksudi.

Kisha RC Homera akazungumzia suala la ukusanyaji wa mapato ambapo ameuasa uongozi kusimamia zoezi hilo vizuri na kutoa ushauri kwa wahudumu kuepuka kutumia simu hasa kuperuzi mitandao ya kijamii wakati wanahudimia wagonjwa.

Katika suala la uwekezaji RC Homera amewaeleza wafanyakazi wa hospitali hiyo kuwa wajitahidi kuwekeza kila wapatapo nafasi ya kupata chochote katika sehemu ya mapato yao kama mishahara na posho ili kuepuka utegemezi katika siku zao za usoni.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya akizungumza na wafanyakazi wa hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya (Picha na Castus bhusolo)

Dkt: Godlove Mbwanji Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya akamshukuru RC Homera kwa kutenga muda wake kuzungumza na wafanyabiashara na kukitaja kitendo hicho kama kitendo cha kiuungwana ambacho viongozi wengine hawafanyagi hivyo.

Wafanyakazi hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera(Picha na Castus bhusolo)