Baraka FM

Marufuku yapigwa uuzaji holela wa viuatilifu

28 March 2024, 19:39

Washiriki wa mafunzo wakifuatilia kwa ukaribu wa mafunzo ya viuatilifu katika ukumbi wa kibo jijini Mbeya(picha na Hobokela Lwinga)

Matumizi sahihi ya viuatilifu yanatajwa Zaidi kuwa sehemu bora ya uzalishaji wa mazao.

Na Hobokela Lwinga

Wasambaji na wakulima Nchini wametakiwa kutumia viutilifu vilivyosajiliwa sambamba na wenye maduka ya viutilifu kujisajili ili kuondoa wimbi la matumizi viutilifu visivyofaa.

Wito huo umetolewa na mratibu wa mafunzo kutoka mamlaka ya afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu Tanzania Jumanne Rajabu Msalama katika semina iliyojumuisha wauzaji wa viuatilifu wa mikoa ya nyanda za juu kusini iliyofanyika jijini Mbeya.

Sauti ya mratibu wa mafunzo kutoka mamlaka ya afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu Tanzania Jumanne Rajabu Msalama

Aidha bw.Msalama amesema kila mfanyabiashara anapaswa kufuata vigezo vya uuzaji wa viuatilifu ikiwa ni pamoja na kujisajili.

Sauti ya mratibu wa mafunzo kutoka mamlaka ya afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu Tanzania Jumanne Rajabu Msalama

Hata hivyo Msalama amewataka Wananchi kitoa taarifa pindi wanapoona uingizwaji na utengenezaji wa viuatilifu kiholela kwani athali zake ni kubwa kiafya kwa badae.

Mratibu wa mafunzo kutoka Mamlaka ya afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu Tanzania Jumanne Rajabu Msalama(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mratibu wa mafunzo kutoka Mamlaka ya afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu Tanzania Jumanne Rajabu Msalama

kwa upande wake mtafiti na mtaalamu wa viuatilifu na visumbufu vya mimea kutoka mamlaka ya afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu Tanzania bw.Maneno Chidege amewataka wauzaji na wakulima kutoa taarifa wakiona kuna wadudu waharibifu kwenye maeneo yao ili utafiti uweze kufanywa na udhibitiwe kulinga na kiuatilifu husika.

Mtafiti na mtaalamu wa viuatilifu na visumbufu vya mimea kutoka Mamlaka ya afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu Tanzania bw.Maneno Chidege(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mtafiti na mtaalamu wa viuatilifu na visumbufu vya mimea kutoka Mamlaka ya afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu Tanzania bw.Maneno Chidege

Nao baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wameishukru mamlaka ya afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu Tanzania kwa kuwaandalia mafunzo hayo ambapo wamesema yamewaongezea mawanda mapana ya kutoa huduma bora na mahususi kwa wakulima.

Sauti ya baadhi ya washiriki wa mafunzo

Mamlaka ya afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu Tanzania imekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali Nchini lengo likiwa ni kuhakikisha matumizi sahihi wa viuatilifu unafuatwa na katika Semina iliyofanyika jijini Mbeya iliyowakutanisha wauzaji wa viuatilifu ilianza jumatatu machi 25 na inatarajiwa kumalizika machi 29,2024.