Baraka FM

Askofu Nyaisonga amtembelea Rc Homera nyumbani kwake

2 January 2024, 18:08

Na mwandishi wetu

Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Katoliki Mbeya na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Gervas Nyaisonga Leo Tarhe 01/01/2024 amefika Nyumbani kwa Cde Juma Zuberi Homera Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa lengo la kumtakia Kheri ya Kumbukizi ya Siku yake ya Kuzaliwa iliyoambatana na Salamu za Christ-mass na Mwaka Mpya.

Mbali na Salamu hizo Nyaisonga amempongeza RC Homera kwa Kazi Nzuri ya kuongoza Mkoa wa Mbeya katika Hali ya Amani na Utulivu.

  “Tunamshukuru Rais Samia kwa kutuletea RC Mchapa kazi na sisi kama Kanisa Katoliki tunatambua saana Kazi yako unayoifanya hapa Mkoani kwetu Mbeya Mwenyezi akulinde na akupe Afya Njema ili uendelee kuungoza vyema Mkoa wetu”

RC Homera amemshukuru Askofu Nyaisonga kwa Ujio wake na kuahidi kuwa Serikali itaendelea Kutoa ushirikiano wa Kutosha kwa Kanisa Katoliki na Madhehebu mengine Kutoka Dini Mbali mbali.