Baraka FM

Tufanye kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi zetu

9 December 2023, 08:16

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Rodrick Mpogolo

Na Hobokela Lwinga

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Rodrick Mpogolo amewataka Watumishi wote Mkoani Mbeya Kufanya Kazi kwa Kufuata Misingi na Maadili ya Kazi na kutanguliza Mbele Uzalendo ili Wananchi wapate huduma sahihi sawasawa na Wanavyostahili.

Ameyasema hayo Wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe .

Mpogolo Amesema”Mimi niwaombe Kila Mmoja asimame kwenye Nafasi yake tuepuke Migogoro isiyo na Sababu Kwani Kuna Shida gani Watumishi wa Afya wakiihudumia Jamii kwa kujitoa kadharika Elimu na Sekta zingine!!?

Ndugu zangu tufanye Kazi kwa Bidii huku tukitanguliza Mbele Maslahi ya Nchi, hakuna Nchi Nyingine utaipata zaidi ya Tanzania na ili tufanikiwe kupiga hatua kama Nchi lazima tutangulize Uzalendo Kwanza” Amesema Mpogolo

Hata hivyo ameipongeza Halmashauri ya Rungwe kufanya Vizuri kwenye Matokeo ya Darsa la Saba kwa kupata Ufaulu wa zaidi ya Asilimia 90 na kuwaomba Walimu waendeleze bidii ili kuiweka Halmashauri kwenye Nafasi Nzuri ya Ufaulu.

Mbali na Kuzungumza na Watumishi RAS Mpogolo ametembelea na Kukagua Ujenzi wa Shule ya Sekondari Mpepo na kuwataka Wasimamizi Kuongeza jitihada ili ifikapo January Wanafunze waanze Masomo.