Baraka FM

Songwe waanzisha mradi wa parachichi kujikwamua kiuchumi

12 December 2023, 19:28

Na mwandishi wetu,Songwe

Ili Kujikwamua kiuchumi na kuanza kujitegemea Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Songwe imeanzisha mradi wa kilimo cha zao la parachichi ambalo wanategemea kuanza kuvuna baada ya miaka miwili.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Songwe Stephano Simbeye desemba 9, kwenye maonyesho ya klabu za habari yaliyofanyika Dodoma kwenye ofisi za umoja wa klabu za waandishi wa Habari nchini (UTPC).

Alisema licha ya Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Songwe kuwa kitinda mimba kwa kuanzishwa, wameamua kuanzisha mradi huo ili ili baada ya miaka miwili uwe chanzo cha kuingiza mapato.

“Mradi huu tulanzisha mwaka 2021 ambapo tulianzisha bustani ya miche, tulipofanikiwa kuiuza tulinunua shamba ekali moja ambalo tumepanda miche yetu tunayotegemea kuanza kuvuna baada ya miaka miwili ijayo” alisema Simbeye.

Rais wa umoja wa vilabu vya Habari nchini Tanzania Deogratus Nsokolo akiongea baada ya kukagua maonyesho yaliyofanywa na klabu za uandishi wa habari kutoka mikoa yote alisema amefurahishwa na namna ambavyo klabu  zimeanza kupiga hatua kutafuta vyanzo vya mapato.

Alisema maonyesho hayo yamekuwa na mafanikio makubwa kwa sababu Viongozi wa klabu za uandishi wa Habari wameweza kubadilishana uzoefu wa kubuni miradi mbalimbali kulingana na maeneo yao.

Naye mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa klabu za uandishi wa Habari nchini Tanzania (UTPC) Keneth Simbaya amesema maonyesho yaliyoonyeshwa na viongozi wa Klabu za waandishi wa Habari yametoa mrejesho mzuri ambao utakwenda kujenga na kuimalisha klabu kuwa imara.

Kwa upande wake Jane Shusa mwakilishi kutoka shirika la Twaweza aliwasihi waandishi kujenga tabia ya kuzisemea changamoto zao hasa za kuwa na masrahi madogi na kukosa mikataba .