Baraka FM

Wakristo watakiwa kuchangia damu kusaidia wagonjwa wenye uhitaji

16 April 2024, 15:28

Mchungaji wa kanisa hilo Pasco Masawili(picha Anna Mbwilo)

Jamiii imetakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwezesha banki ya damu kuwa na akiba ya kutosha.

Na Anna Mbwilo

Waumini wa kanisa la TAG Nzovwe jijini Mbeya wametakiwa kuchangia damu kwa lengo la kuiwezesha benki ya damu kuwa na akiba ya kutosha ili kusaidia watu mbalimbali wanaohitaji kuongezewa huduma hiyo.

Hayo yamesemwa na Mchungaji wa kanisa hilo Pasco Masawili wakati akizungumzia umuhimu wa kuchangia damu katika kuelekea maadhimisho ya miaka 85 ya kanisa la TAG nchini na miaka 51 ya kanisa la TAG Nzovwe.

Mch. Masawili amesema kuwa zoezi la uchangiaji damu ni sehemu ya kuwasaidia wahitaji kwa kuwa suala hilo ni la kiroho na kiimani.

Sauti ya Mchungaji wa kanisa T.A.G Nzovwe Pasco Masawili

Nae katibu wa kanisa hilo Aggyley Nzingana amesema wameamua kuungana pamoja kuchangia damu kwa lengo la kuigusa jamii huku akiwashukuru waumini kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo.

Sauti ya katibu wa kanisa T. A. G Nzovwe Aggyley Nzingana

Kwa upande wao baadhi ya waumini wa kanisa hilo wameeleza kufurahishwa na hatua ya wao kuchangia damu huku wakiushukuru uongozi wa kanisa kwa kuwahamasisha kuchangia damu ili kusaidia jamii.

Sauti za waumini wa kanisa la T. A. G Nzovwe

Hata hivyo mratibu wa huduma za maabara jiji la Mbeya Elia Isaya ameushukuru uongozi wa kanisa la TAG Nzovwe kwa kuchangia damu huku akiwataka wananchi kuachana na Imani potofu kuhusu uchangiaji damu.

Sauti ya mratibu wa huduma za Maabara jiji la Mbeya Elia Isaya