Baraka FM

TAKUKURU Mbeya yakagua miradi 53 yenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 177.

1 June 2026, 18:03

Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, Jasper Luoga(picha na Hobokela Lwinga)

Ushirikiano wa wananchi ni muhimu katika kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa, hivyo kila mwananchi anapaswa kutoa taarifa kwa wakati ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Na Hobokela Lwinga

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya, imekagua miradi 53 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 177 kwa lengo la kuhakikisha inatekelezwa na kukamilika kwa thamani halisi ya fedha zinazotolewa.

‎‎Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TAKUKURU kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi 2026, Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, Jasper Luoga, amesema uchambuzi na ufuatiliaji wa miradi hiyo umeonesha dosari mbalimbali zinazohitaji kufanyiwa kazi ili kuhakikisha thamani ya fedha za umma inalindwa.‎‎

Sauti ya Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, Jasper Luoga

Aidha, amesema katika kipindi hicho TAKUKURU imefanikiwa kuokoa mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 150 zilizokuwa zinahusiana na kikundi cha Asante Mbeya Project, hatua ambayo imechangia kulinda maslahi ya kikundi.‎‎

Sauti ya Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, Jasper Luoga

Katika hatua nyingine, Luoga amesema TAKUKURU itaendelea kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa kupitia utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii,Ameeleza kuwa katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2026, taasisi hiyo itatoa elimu kwa wanafunzi, wananchi na watumishi wa umma kuhusu athari za rushwa na umuhimu wa kujiepusha na vitendo vya rushwa.‎‎

Sauti ya Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, Jasper Luoga