Nuru FM

Jamii Iringa yaaswa kushiriki katika malezi

11 May 2026, 13:06

Katibu wa Shughuli za Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Iringa, Bi. Olumbi Makala akizungumza kuhusu malezi. Picha na Joyce Buganda

Na Joyce Buganda

Jamii Mkoani iringa imetakiwa kuongeza ushirikiano katika malezi ya watoto ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao na kulindwa dhidi ya changamoto zinazowakabili.

Wito huo umetolewa na Katibu wa Shughuli za Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Iringa, Bi. Olumbi Makala, wakati wa kikao cha pili cha maandalizi kuelekea kilele cha siku hiyo huku akiisistiza kuwa malezi ya mtoto yanahitaji nguvu ya pamoja

Sauti ya Makala

Akizungumzia hali ilivyo mitaani, Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Kihesa, Bi. Rebeca Lugenge, amebainisha kuwa changamoto kubwa iliyopo ni mmomonyoko wa maadili na utoro wa wanafunzi.

Sauti ya Rebeca

Kwa upande wake, mwakilishi wa kituo cha kulelea watoto cha Consolata Nyumba ya Furaha, Bi. Agnes Mbilinyi, amesema elimu hiyo itasaidia vituo kuboresha mazingira ya kuishi kwa watoto na kuwajenga katika maadili mema.

Sauti ya Mbilinyi

Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kitafanyika kitaifa na kimkoa mnamo Juni 16, 2026, ambapo kwa Manispaa ya Iringa, sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Mwembetogwa.