Baraka FM
Baraka FM
10 July 2025, 16:01

Kwenye maisha usiwe mtu wa kujisifu badala yake acha kazi yako na bidii yako ikutambulishe kwa watu,ndio hapo utasifiwa na wanao ona.
Na Hobokela Lwinga
Wananchi katika kijiji cha Nsonyanga A kata ya Mahongole wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wameishukru serikali kupitia kwa diwani wa kata hiyo Patrick Mwaisoba kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wakizungumza na kituo hiki baada ya kutembelewa katika Kijiji cha Nsonyanga wananchi hao wamesema diwani wao amekuwa chachu kubwa ya maendeleo
Erica Mbogela ni mwananchi,amesema diwani wao huyo katika uongozi wake imefanikisha ujenzi wa shule ya Sekondari Shamlindima hali iliyosaidia wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu katika shule ya Sekondari Ruiwa Iliyopo nje ya kijiji chao.

Nae mwenyekiti wa Kijiji cha Nsonyanga A Gasper kalinga ameishukru serikali kwa kutoa ushirikiano wa kufanikisha maendeleo kupitia uongozi wao katika sekta mbalimbali za elimu,afya na maji.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya shule ya Sekondari Shamlindima,ambaye pia ni mchungaji wa ushirika wa Nsonyanga Amos Mwangole amesema wao kama viongozi wa dini wamekuwa chachu ya ujenzi wa Shule mpya tangu ujenzi wake kuanza hadi ulipofikia sasa.

Hata hivyo kituo kimetafuta Diwani huyo wa kata ya Mahongole anayemaliza muda wake mhe. Patrick Mwaisoba amesema mafanikio yake kwenye uongozi wake yametokana na ushirikiano anaoupata kutoka kwa wananchi
