Wananchi watakiwa kuacha kuchoma moto wakati wa kuandaa mashamba
9 October 2024, 08:24
Wakati msimu wa kilimo ukiwa umekaribia wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhali ya kutokuharibu Mazingira.
Na Hobokela Lwinga
Wito umetolewa kwa baadhi ya wananchi kuacha tabia ya kuchoma moto mashamba wakati wa usafishaji ili kuepuka athari za moto huo kusambaa katika maeneo mengine hasa misitu.
Akizungumza Na kituo hiki Innocent Lupembe wakala wa huduma za Misitu (TFS) Kanda Ya Nyanda Za Juu Kusini, amesema matukio ya moto yanatokea kila mwaka hasa kiangazi, kutokana na baadhi ya wakulima kuchoma moto mashamba yao wakati wa usafishaji hali inayosababisha uharibufu wa misitu hiyo.
Hata hivyo amesema wamekua wakishirikiana na wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka misitu kwa kuwapa elimu ya namna ya kudhiti moto pindi ukitokea, pamoja na kulinda misitu hiyo kwa ujumla.
Katika hatua nyingne Lupembe ameonya boda boda wanautumia vyombo hivyo kusafirisha mkaa,akisema Serikali haijaruhusu usafiri huo kutumika,kwani pia ni hatari kwa watumiaji wa barabara.