Baraka FM

Mch. Sinkwembe aongoza ibada ya ‘jenga wilaya’ Mbeya

15 March 2026, 15:32

Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi wilaya ya Mbeya mchungaji Greenwell Sinkwembe(picha na Hobokela Lwinga)

Kutoa sadaka kwa ajili ya kujenga madhabahu ni jambo muhimu katika kuifanya kazi ya Mungu kwa sababu madhabahu ni mahali pa kumtolea Mungu ibada.

Na Hobokela Lwinga

Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi wilaya ya Mbeya mchungaji Greenwell Sinkwembe ameongoza ibada ya uzinduzi wa ibada ya Jenga wilaya.

‎Ibada hiyo imefanyika machi 15,2026 katika Kanisa la Moravian Ushirika wa Nzovwe lililopo jijini Mbeya, na kuhudhuriwa na waumini mbalimbali wa kanisa hilo.

‎Akihubiri katika ibada hiyo, Mchungaji Sinkwembe amewahimiza Wakristo kuwa na moyo wa utoaji katika kuendeleza kazi ya Mungu.

‎Mwenyekiti huyo amesisitiza kuwa utoaji ni sehemu muhimu ya imani ya Kikristo na unasaidia katika kujenga na kuimarisha huduma za kanisa pamoja na kuendeleza miradi ya maendeleo ya kiroho na kijamii.

Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi wilaya ya Mbeya mchungaji Greenwell Sinkwembe(picha na Hobokela Lwinga)


‎Aidha, amewakumbusha waumini umuhimu wa kuyakumbuka matendo makuu ya Mungu aliyowatendea katika maisha yao, Amesema kuwa kumkumbuka Mungu kwa matendo yake mema humsaidia Mkristo kuwa na shukrani, imani thabiti na moyo wa kujitoa zaidi katika kumtumikia Mungu.

Baadhi ya waumini walioshiriki ibada katika kanisa la Moravian ushirika wa Nzovwe (picha na Hobokela Lwinga)

‎Katika ibada hiyo, litrujia imeongozwa na Mchungaji wa Ushirika wa Nzovwe, Mchungaji Jonam Msangawale.

Mchungaji wa Ushirika wa Nzovwe, Mchungaji Jonam Msangawale(picha na Hobokela Lwinga)



‎Vilevile, katika shirika zote zinazounda Kanisa la Moravian Wilaya ya Mbeya, waumini wamefanya ibada ya Jenga Wilaya kwa pamoja kwa kutoa sadaka maalumu ya ujenzi.