Baraka FM
Baraka FM
15 October 2025, 16:52

Wakuu wa taasisi binafsi na serikali wametakiwa kuwanufaisha wasajili wao na Mfuko Hifadhi ya Jamii wa Taifa (NSSF).
Na Hobokela Lwinga
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Beno Malisa amewataka waajiri kutimiza takwa la kisheria la kuwasajili wafanyakazi wao katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa (NSSF) kwa manufaa ya wafanyakazi huku akiwataka wakuu wa wilaya mkoani humo kuhakikisha wanasimamia zoezi hilo kwa ukaribu.
Ameyasema hayo wakati akikabidhi mitungi zaidi ya 100 kwa Mamalishe na babalishe yaliyotolewa na NSSF ikiwa ni sehemu yakurudisha kwa jamii ambapo amesema sheria inaruhusu kutumia nguvu za ziada kuhakikisha waajili wanatimiza takwa hilo.
Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa (NSSF) Masha Mshomba anaeleza baadhi ya huduma zilizoboreshwa katika Mfuko huo huku mmoja wa wanufaika akieleza namna alivyonufaika na mfuko huo.
