Baraka FM

Watu kadhaa wahofiwa kufariki katika ajali nyingine Mbeya

27 July 2025, 19:37

Baadhi ya mashuhuda wakishuhudia ajali Nzovwe Mbeya

Jinamizi la ajali limeendelea kuukumba mkoa wa Mbeya.

Na Hobokela Lwinga

Ajali hiyo imetokea leo Julai 27, ambapo kituo hiki kimefika katika maeneo hayo na kushuhudia Jeshi la Polisi, Zimamoto na wananchi wakisaidia kuokoa baadhi ya majeruhi na kutoa miili ya waliofariki dunia.

Watu kadhaa ambao bado idadi yao haijajulikana wanahofiwa kufariki dunia katika ajali maeneo ya mteremko wa Nzovwe hadi kwenye daraja la Iyunga kunakoendelea ujenzi wa barabara ya njia nne jijini Mbeya ikihusisha magari matano.

Ajali ya kwanza imehusisha gari la abiria linalofanya safari zake Mbalizi – Nsalaga, lori na tipa la mchanga kwa upande wa eneo la Nzovwe.

Kwa upande wa eneo la Iyunga, imehusisha gari aina ya Coasta inayofanya safari kati ya Mbalizi – Standi Kuu, Lori lililokuwa na shehena ya saruji na mengineyo ambayo hayakutambulika haraka.