Baraka FM

Mwanamke afariki kwa kuungua moto Mbeya

22 July 2025, 12:52

Jeshi la zimamoto na uokoaji wakiingiza mwili wa marehemu kwenye gari(picha na Deus Mella)

Katika hali ya kushangaza mwanamke mmoja amekutwa amefariki ndani katika tukio linalodhaniwa chanzo ni mgogoro wa ardhi.‎‎

Na Deus Mella

Mwanamke mmoja ajulikanaye kwa jina la Luth Mtawa mkazi wa mtaa wa Majengo B kata ya Kalobe mkoani Mbeya amekutwa amefariki kwa moto ndani ya nyumba yake huku chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.‎‎

Tukio hilo limetokea limetokea usiku wa kuamkia leo julai 22, 2025.

‎‎Baadhi ya mashuhuda wanasema hili ni tukio la kushangaza na limeleta taharuki kubwa kwao.‎‎

Nae mwenyekiti wa mtaa wa Majengo B amesema hili ni tukio la pili kutokea ndani ya mtaa wake huku akiwataka wananchi kuwa watulivu kipindi hiki ambacho uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo.‎‎

Tayari jeshi la Zima moto na uokoaji wamefika katika eneo la tukio na kuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi.

Hii ni nyumban ya marehemu aliyekuwa akiishi(picha na Deus Mella)