Baraka FM

Afisa elimu mstaafu Mwashusa achukua fomu kugombea udiwani kata ya Nsalala

30 June 2025, 16:17

Picha ya Petro Jacobo Mwashusa (Kulia)na Rukia Chasanika

Wakati pilikapilika za uchaguzi zikiwa zinaendelea watia nia hususani wa chama cha mapinduzi wameendelea kuchukua fomu kuomba ridhaa ya kuwania nafasi za ubunge na udiwani kwenye maeneo yao.

Na Rukia Chasanika

Zoezi la uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi za kugombea nafasi za ubunge na udiwani linaendelea katika chama cha mapinduzi (CCM) nchini kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 2025.

Petro Jacobo Mwashusa ni mmoja wa wanachama wa chama hicho waliojitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya udiwani katika kata ya Nsalala iliyopo katika mji mdogo wa Mbalizi mkoani Mbeya.

Mwashusa amesema endapo atapitishwa kugombea nafasi hiyo ya diwani kata ya Nsalala na kuchaguliwa na wananchi atahakikisha anasimamia miradi yote inakamilika kwa wakati pamoja na kusimamia rasilimali fedha za kata hiyo.

Sauti ya Petro Jacobo Mwashusa

Petro mwashusa amesema ameongoza walimu Zaidi ya elfu sita hivyo ana uwezo wa kutumikia wananchi kwa kusimamia vizuri rasilimali fedha katika kata hiyo.

Sauti ya Petro Jacobo Mwashusa

Kwa upande wake mpambe wa Emmanuel Mumbii aliyemsindikiza kuchukua fomu amesema Petro Mwashusa ni mtu sahihi kuwania nafasi hiyo kutokana na sehemu alizofanya kazi akiwa kiongozi katika ngazi mbalimbali maeneo tofauti nje na ndani ya chama cha mapinduzi.

Sauti ya mpambe Emmanuel Mumbii

Petro Jacobo Mwashusa ni mwalimu mstaafu aliyestaafu akiwa afisa elimu wa halmashauri ya sumbawanga mkoani Rukwa.