Baraka FM
Baraka FM
17 June 2025, 19:06

Wadau na taasisi mbalimbali wameombwa kutowatenga wahitaji badala yake wanatakiwa kujenga utamaduni wa kuwatembelea na kuwasaidia wahitaji misaada mbalimbali kwani kufanya hivyo ni sadaka na thawabu mbele za Mungu.
Na Hobokela Lwinga
Watu wenye ulemavu wametakiwa kutumia fursa za elimu ya ujariamali wanazozipata ilikuweza kujiinua kiuchumi hali itakayowaondolea utegemezi.
Rai hiyo imetolewa na Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Robert Pangani wakati akifunga semina ya watu wenye ulemavu katika halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya iliyoandaliwa na idara ya udiakonia katika kanisa hilo iliyofadhiliwa na mission 21.
Askofu Pangani amesema kuwa mlemavu hakuondoi uwajibikaji wa kuzalisha mali.

Kwa upande wake mwakilishi wa serikali katika halmashauri ya wilaya ya Mbarali, ambaye ni afisa mazingira bw.Raphael Shitindi amesema serikali inaendelea kuweka mazingira Mazuri kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na fursa za mikopo isiyo na riba ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri.
Aidha akitoa taarifa Mbeya ya wageni na washiriki, Katibu idara ya udiakonia kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi bw.Eliud Mahenge amesema lengo la kuanda mafunzo hayo kwa watu wenye ulemavu ni kuwawezesha kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye jamii.

Hata hivyo akizungumza mwakilishi wa shirika la mission 21 Adriane sweetman amesema wataendelea kutoa ushirikiano kwa kanisa katika kuratibu uwezeshaji wa makundi ya watu wenye ulemavu kwani lengo lao ni kuwawezesha watu hao kiuchumi na kiafya.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamewashukru wafadhiri likiwemo kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi, mission 21 kwa kuona umuhimu wa kufanya mafunzo kwa wetu wenye ulemavu.
Katika ufungaji wa mafunzo hayo Baraka fm radio imetunukiwa cheti cha heshima kwa kutambua mchango wa uandaaji wa maudhui ya kupigania haki za watu wenye ulemavu kilichotolewa na Shirika la Tanzania Joy Women Entrepreneurship for the Deaf (FUWAVITA) lenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam.
