Baraka FM
Baraka FM
9 June 2025, 15:09

Kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi limeendelea kutoa elimu kwenye taasisi na idara zake kuhusu umuhimu wa kufanya matendo ya huruma yaani udiakonia.
Na Hobokela Lwinga
Walezi na wahudumu wa watoto katika vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima na watoto wenye mahitaji maalumu wamekumbushwa wajibu wao katika kuwalea watoto kwenye misingi ya neno la Mungu.
Rai hiyo imetolewa na makamu mwenyekiti kanisa la Moraviani Tanzania jimbo la kusini magharibi Asulumenye Mwahalende wakati akifungua semina ya udiakonia yenye lengo la kutoa Elimu ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi, Semina hiyo imefanyika katika kituo cha watoto ya tima Cha Amani Nsalaga kilichopo jijini Mbeya.

Nae katibu wa Idara ya udiakonia katika kanisani la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ndugu Eliudy Mahenge Ameeleza lengo la Idara ya Udiakonia kuwa ni kutoa huduma kwa wahitaji.

Aidha Afisa Afya Idara ya Udiakonia wa kanisa la Moraviani Tanzania jimbo la kusini magharibi Emmanuel Angetile Ameitaka jamii kutokuwabagua watoto kwani watoto hao ni msaada kwa ajili ya wakati ujao.

Hata hivyo mkufunzi katika semina hiyo Ambaye ni mhudumu wa afya nasihi Juliana willa amewakumbusha wazazi na walezi wa watoto kutoa malezi Bora kwa watoto wao ili kuepukana na makundi rika.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa semina hiyo,msimamizi wa kituo cha watoto yatima Amani Nsalaga Mch.Elizabeth Nampasa amesema elimu waliyoipata itakuwa msaada kwao kwa ajili ya kutoa malezi Bora kwa watoto wanaowahudumia.
