Baraka FM
Baraka FM
26 May 2025, 15:31

Kutokana na uwepo wa uzalishaji maudhui mbalimbali katika mitandao ya kijamii waandishi wa habari wametakiwa kutumia taaluma Zao kuelimisha jamii
Na Ezra Mwilwa
Mafunzo hayo yaliyo andaliwa na mtandao wa Radio Jamii (TADIO) yamefanyika katika ukumbi wa hotel ya Mdope jijini mbeya Amua Rushita ambaye ni Afisa Tehama wa mtandao wa radio jamii amesema nimuhimu sana Redio kutumia mfumo wa radio jamii ili kusaidia usikivu katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.

Mratibu wa mafunzo hayo kutoka TADIO Fatuma Mahendeka amesema wameanda mafunzo hayo kwa siku mbili ili kukumbushana namna ya uandishi Bora wa habari za kuelimisha jamnii nzima.

Nao baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo wamesema mtandao wa radio jamii tangu kuanzishwa kwake umekua na msaada mkubwa hasa katika kuifikia jamii