Baraka FM
Baraka FM
19 May 2025, 16:52

Ni jukumu la kila mwananchi kuombea taifa ili liendelee kuwa na amani na katika hilo kila mtu anaowajibu wakulinda amani ya nchi.
Na Hobokela Lwinga
Waumini Wakanisa La Moravian Tanzania Ushirika Wa Nsonyanga Uliopo Halmashauri Ya Mbeya Wamefanya Ibada Ya Kuliombea Taifa Kuelekea Uchaguzi Mkuu October,2025.
Ibada Hiyo Imeongozwa Na Mchungaji Wa Ushrika Wa Nsonyanga Amosi Mwangole Huku Ikihudhuliwa Na Viongozi Wa Serikali Wakiongozwa Na Diwani Wa Kata Ya Mahongole Mhe.patrick Mwaisoba.
Akizungumzia Umuhimu Wa Kuombea Taifa Mchungaji Amesema kanisa kazi yake ni kuomba nyakati zote pia amesistiza uwepo wa uchaguzi wa haki na amani.
Aidha mchungaji Mwangole amewataka wananchi kwenda kupiga kula ya kumchagua kiongozi wanayemtaka ili aweze kuwaongoza.

Nae Diwani Wa Kata Ya Mahongole halmashauri ya wilaya ya Mbarali Mhe. Patrick Mwaisoba ameomba Kanisa Liendelee Kuliombea Taifa Kwani Kila Mamlaka Inayongoza Taifa lolote duniani Inatoka Kwa Mungu huku akilishukru kanisa kwa kutambua umuhimu wa kuliombea taifa.

Baadhi Ya Waumini Walioshiriki Ibada Hiyo Wamesema wanamuomba mungu awarejeshee viongozi wote waliofanya kazi vizuri katika utendaji wao uchaguzi ujao mwaka huu 2025.
