

7 March 2025, 09:55
Wahenga wanasema nyumba bila wageni hiyo sio nyumba,ishara ya kutembelewa na wageni ni kuonyesha upendo wa namna unavyoishi na watu.
Na Hobokela Lwinga, Mbeya
Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi limewapokea na kuwaaga wageni kutoka nchini Ujerumani waliofika nchini kulitembelea jimbo na kanisa kwa ujumla.
Wageni waliofika nchini kutokea Nchini Ujerumani ni Michael Gutekunst na Jurgen Bernhardt.
Wakiwa nchini Tanzania na baada ya kufika katika kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi waliweza kutembelea taasisi za kanisa ikiwemo Radio Baraka fm pamoja na chuo cha ufundi Moravian Mbeya taasisi zilizopo kadege jijini Mbeya wakiongozwa na mwakilishi wa kamati tendaji ya KMT-JKM Ambaye ni Mkurugenzi wa idara ya miradi na uchumi Ndugu Essau Swila.
Aidha wageni hao wameahidi kuendeleza ushirikiano ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto ambazo zinazozikabili taasisi za kanisa.
Akizungumza na wageni hao ofisini kwake, meneja wa redio Baraka fm Charles Amlike aliwaeleza namna kituo hicho kinavyorusha matangazo hayo ikiwa ni sambamba na matumizi ya masafa pamoja na njia ya mtandao.
Wageni hao wameondoka kurudi kwao Ujerumani na wameagwa na viongozi wandamizi wa kanisa wakiongizwa na Baba Askofu Robert Pangani ambaye pia ni mwenyekiti wa jimbo pamoja na makamu mwenyekiti na Kaimu Katibu Mkuu Mch.Asulumenye Mwahalende.