

10 February 2025, 22:41
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera ametembelea shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Holly Land iliyopo Mamlaka ya Mji Mdogo wa Makongolosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Lengo la kutembelea shule hiyo ni kuipongeza kwa matokeo mazuri tangu kuanzishwa kwake na uwekezaji mkubwa wa Lawena Nsonda(Baba Mzazi).
Aidha amewataka wazazi Mkoani Mbeya kuwapeleka watoto shuleni hapo badala ya kuwapeleka mbali kwani shule ina huduma nzuri na malezi mazuri.
Kwa upande wake Lawena Nsonda (Baba Mzazi) ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa kwa wawekezaji nchini wakiwemo wamiliki wa Shule.
Shule ya Holly Land ni moja ya shule bora zinazofa vema Kiwilaya,Kimkoa na Kitaifa.