Moravian Mbozi yatoa ushirikiano wa utendaji Jimbo la Magharibi
26 November 2024, 05:49
Ili uwe Bora ni lazima ukubali kujifunza kwa wengine hii ndio maana halisi ya mafanikio katika nyanja mbalimbali katika maisha.
Na Deus Mellah
kanisa la Moraviani Tanzania jimbo la magharibi Tabora wamefanya ziara ya kujifunza mfumo rafiki wa kuinua mapato ya ndani ya kanisa katika majimbo ya kusini, jimbo la kusini magharibi na jimbo la Mbozi.
Akizungumza na viongozi wa jimbo la mbozi katibu mkuu wa kanisa la moravian Tanzania jimbo la magharibi (Tabora) Mch Richard Rwali amesema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwa sababu wameona jinsi ya majimbo mengine wanavyoweka mchanganua wa makisio.
Naye mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Magharibi wilaya ya kati Sikonge Benjemin Kamage amewaomba wakristo wa jimbo la Magharibi kukubali mfumo mpya wa mabadiliko na kupokea vitu vipya.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kanisa la Moravian jimbo la Mbozi Mch Lawrance Nzowa amewashukuru viongozi hao kwa kufanya ziara katika jimbo lao kwani wamebadilishana uzoefu juu ya utendaji kazi katika kanisa.
Pia amewaomba wakristo wa jimbo la Mbozi kuendelea kuliombea kanisa na kuliombea taifa na viongozi wa nchi.