Baraka FM

Tigo, serikali kushirikiana kuhudumia wananchi huduma za kifedha

23 October 2024, 16:05

Serikali ikiendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji nao wanawajibu wa kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Na Hobokela Lwinga

Kampuni ya mawasiliano Tanzania Tigo imesema itaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali kuhudumia wananchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo kupitia huduma za kifedha.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa operation za huduma za Tigo pesa Arnold Ngalashi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya huduma za kifedha kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ruanda nzovwe jijini Mbeya.

Sauti ya mkurugenzi wa operation za huduma za Tigo pesa Arnold Ngalashi

Ngalashi amesema mbali na huduma ya tigo pesa pia wanahuduma ya vicoba inayosaidia vikundi mbalimbali kuweka fedha kuwa salama na kuongeza uwazi kwa wanakikundi.

Sauti ya mkurugenzi wa operation za huduma za Tigo pesa Arnold Ngalashi

Sambamba na hayo mkurugenzi huyo amesema kampuni yake imewasaidia wakulima kupata malipo mbalimbali katika uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Sauti ya mkurugenzi wa operation za huduma za Tigo pesa Arnold Ngalashi

Katika hatua nyingi amewataka wananchi kuendelea kutumia mtandao wa tigo kwani umekuwa karibu na wao katika kuwezesha huduma za mawasiliano nchini.