Watahiniwa kidato cha nne 2024 watakiwa kujiandaa kwa bidii kufanya mtihani wa taifa
17 October 2024, 21:11
Wakati wahenga wanasema elimu haina mwisho hii inamaana kwamba unapotoka hatua moja inakupeleka hatua nyingine ya elimu ya juu.
Na Deus Mellah
Wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kufanya mtihani wao wa taifa Novemba 11, 2024 wametakiwa kujianda na kupitia mara kwa mara yale waliyofundishwa na walimu wao ili waweze kufanya vizuri mtihani huo.
Wito huo umetolewa na mkuu wa shule ya wasichana solace Roda Basili wakati akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo kuhusu wanafunzi kuongeza bidii katika masomo yao ilim waweze kufaulu mtihani huo wa taifa.
Amesema kama walimu wa shule hiyo wanapambana ili kuhakikisha wanafunzi wa shule hiyo wanaoenda kufanya mtihani wanatimiza malengo yao.
Mmoja wa walimu shuleni hapo John Komba amewataka wanafunzi hao kuendelea kujifunza zaidi na tabia njema hapo watakapomaliza masomo yao ya kidato cha nne.
Nao baadhi ya wanafunzi wamesema wamejianda sana na mtihani huo wa Taifa na wanahakikisha wanasoma kwa bidii.