Moravian, St.Galen la Uswisi kushirikiana kusaidia wenye mahitaji maalum
8 October 2024, 01:04
Ili uweze kufanikiwa kwenye jambo lolote ni lazima uhitaji ushirikiano kutoika kwa mtu mwingine iwe kimwili au kiroho ndio maana wahenga wanasema “kidole kimoja hakivunji chawa“.
Na Deus Mellah
Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi limeanzisha ushirikiano na kanisa la Uinjilisti St galen kutoka nchini Uswisi lengo likiwa ni kueneza injili katika nchi hizo na kuwafikia watu wenye mahitaji maalumu.
Akizungumza katika ibada maalumu iliyofanyika kanisa la Moraviani ushirika wa Mabatini Askofu wa kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi Robert Pangani amewataka Wakristo kuendeleza umoja huo na kushikamana.
Askofu Pangani amesema kwa sasa kanisa la Moraviani linazidi kuwa kubwa hivyo wanafikilia kufungua misheni ya Chunya.
Kwa upande wake Mch. Anne Ditrich kutoka makanisa ya uinjilist st galen nchini uswisi amesema wamekuja kuanzisha ushirikiano huo ili kuleta mafanikio kwa pande zote.
Naye katibu mkuu wa Kanisa la Moraviani Jimbo la Kusini Magharibi Israel Mwakilasa amesema ushirikiano huo utasaidia kuwahudumia na kuwafikia watu wenye mahitaji maalumu.