Baraka FM

Mahakama kuu Tanzania kanda ya Mbeya yazindua mahakama inayotembea

5 October 2024, 09:55

Uzinduzi wa mahakama inayotembea (picha na Deus Mellah)

Wakati jamii ikihitaji kupata huduma za ukaribu kwenye maeneneo yao,mahakama kuu ya Tanzania imeanza kutoa huduma hiyo kwa kutoa huduma kupitia gari ambayo itazungunguka kwenye maeneo yao.

Na Deus Mellah

Mahakama kuu ya  Tanzania kanda ya Mbeya imezindua  mahakama inayotembea yaani mobile Court Services itakayorahisisha kutoa huduma kwa wananchi wa maeneo mbalimbali.

Wakati wa uzinduzi wa Mahakama hiyo inayotembea  iliyozinduliwa katika stendi ya mabasi Mbalizi mkuu wa mkoa wa Mbeya  Juma Homera ameishukuru Mahakama hiyo kwa ubunifu kwani  wamesogeza huduma kwa wananchi.

Baadhi ya viongozi wa mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera(wa pili kutoka kulia waliamua)-picha na Deus Mellah
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Mbeya  Juma Homera

Homera ametoa wito kwa wananchi wa  mkoa wa mbeya kuitumia mahakama hiyo inayotembea kwani haki itaendelea kwa wananchi wa mkoa wa mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Juma Homera(picha na Deus Mellah)
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Mbeya  Juma Homera

Naye Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Mbeya Joackim Charles Tiganga  watu wengi wanayonafasi ya kuifikia mahakama hiyo na kupata huduma kwa muda mfupi sana.

Sauti ya Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Mbeya Joackim Charles Tiganga

Baadhi ya wananchi mkoani mbeya wameiomba mahakama kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu   ujio wa mahakama inayotembea.

Baadhi ya wananchi mkoa wa mbeya wakiwa katika viunga Vya uzinduzi wa mahakama inayotembea Mbalizi Mbeya (picha na Deus Mellah)
Sauti za baadhi ya Baadhi ya wananchi mkoani mbeya