Wakristo wahimizwa kuliombea taifa juu ya ukatili
17 September 2024, 19:55
Tanzania ni nchi ya amani na kila mwananchi anapaswa kuwa mlinzi wa kulinda amani ya taifa.
Na Hobokela Lwinga
Mchungaji Daniel siame wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi amesema kanisa Lina wajibu wa kukemea na kuombea taifa ili liweze kuondoka na vitendo Vya ukatili ikiwemo utekaji na mauaji ambavyo vinaendelea kwa sasa.
Mchungaji siame ameyasema hayo Wakati akihubiri katika ibada yake ya shukrani iliyoambatana na kuaga katika ushirika wa Ivumwe Moravian.
Katika hatua nyingine amewataka wakristo kushiriki uchaguzi kwa kuchukua fomu za kugombea sambamba na kujitokeza kwa vingi kupiga kura.
Aidha mchungaji siame amelishukru kanisa kwa kuendelea kutumika mahali mbalimbali
Mchungaji wa ushirika wa Ivumwe Rodrick kaponda Amesema mchungaji siame ni mshirika wa Ivumwe hivyo wanamtakia kila la heri katika utumishi wake.
Aidha wakati akizungumzia kituo Cha redio Baraka Meneja wa redio hiyo amesema kituo chake kimekuwa na msaada mkubwa hasa kuwasaidia Watu kukua kiroho na kimwili ikiwemo pia kufunguliwa.