Baraka FM

Watu 11 wafariki dunia, 44 wajeruhiwa ajalini Lwanjilo Mbeya

6 September 2024, 14:47

Hili ndilo gari lilipata ajali katika eneo la Lwanjilo katika halmashauri ya Mbeya mkoani Mbeya (picha na mwandishi wetu)

Siku chache zimepita tangu ajali mbaya kuukumba mkoa wa Mbeya ambapo watu 9 walifariki na 18 kujeruhiwa, wakati maumiv hayo yakiwa bado hayajapoa kwa ndugu waliopoteza wapendwa wao ajali nyingine inatokea ikiwa ni ndani ya mwezi September,2024.

Na mwandishi wetu

Watu 11 wamepoteza maisha na wengine 44 wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya A-N Coach kupata ajali katika eneo la Lwanjilo halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Ijumaa, Septemba 6, 2024 baada ya basi hilo lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Tabora kupinduka wakati likilikwepa lori, kisha kutumbukia mtaroni.

Mganga wa Mkuu wa Hosptali ya Wilaya ya Chunya, Dk Darson Andrew amethibitisha kupokea idadi hiyo na vifo huku akieleza kati ya majeruhi 44 wanne wana hali mbaya na watapewa rufaa kupelekwa Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya ili azungumzie ajali hiyo zinaendelea.