Baraka FM

Watumishi wa afya watakiwa kutoa huduma kwa weledi

27 August 2024, 16:34

Utunzaji miundombinu ni kazi ya kila mtu ili iweze kutumika kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Na Hobokela Lwinga

Kituo cha afya cha kata ya Kiwira Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kimewekwa jiwe la msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg: Godfrey Mnzava na kuwataka wataalam kuwa waaminifu katika utoaji huduma huku wananchi wakiaswa kuitunza miundombinu ya kituo hicho ili kiwafae wao na uzao wao.

Kituo hicho kinachojengwa kimegaharimu kiasi cha Shilingi 500,000,000 fedha kutoka serikali kuu ambapo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za wananchi ambao wao ndio walianzisha kazi hiyo ya ujenzi na hadi kukamilika kwa ujenzi wake kiuo kinatarajiwa kugharimu jumla ya fedha 558,271,594.

Mradi huu unajengwa kupitia mfuko wa manunuzi(Force Account) ambapo Miundombinu inayojengwa ni Pamoja na Jengo la Maabara Jengo pacha la Wazazi na upasuaji, kichomea taka, Jengo la kufulia choo Cha Wagonjwa wa Nje Pamoja na Jengo la Wagonjwa wa Nje.

Mradi Ulianza Kutekelezwa mnamo Tarehe 1/12/2023 na ilitarajiwa Kukamilika Tarehe 30/05/2024 ingawa mpaka Sasa haujakamilika na hii ni kutokana na Changamoto za Mifumo ya Malipo Kushindwa kufanya Kazi kwa Wakati Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Rungwe imeeleza.

Mwenge wa Uhuru Unaendelea na Ziara ya kumulika Miradi Mbalimbali Mkoani Mbeya mpaka Tarehe 30 ambapo utakabidhiwa Mkoani Songwe Tarehe august 31,2024.